Articles by "HABARI ZA BIASHARA"
Showing posts with label HABARI ZA BIASHARA. Show all posts
Mkuu wa kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim Bw. Silas Matoi, akizungumza na mmoja wa washindi wakati wa droo ya kwanza ya kampeni ya Chanja Kijanja, Dili ndio Hili iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Kupitia kampeni hii, wateja wanaotumia kadi za Exim kulipia bidhaa au huduma wanapata nafasi ya kushinda zawadi ya pesa taslimu TZS 100,000 kila wiki, TZS 200,000 kila mwezi, pamoja na zawadi kubwa za TZS milioni 15, milioni 10 na milioni 5 mwisho wa kampeni.Kushoto ni Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim Benedict Mwinula, pamoja na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Rodgers Biteko (kulia), jijini Dar es Salaam.
Droo ya kwanza ya kampeni ya Chanja Kijanja, Dili ndio Hili imeibua washindi watano wa Sh. 100,000 kila mmoja! Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim, Bw. Silas Matoi, aliwatangaza washindi huku akisisitiza kuwa hii ni mwanzo tu.

“Kila wiki, washindi watatangazwa, na kila mwezi washindi 10 watashinda Sh. 200,000. Vilevile, washindi wa droo kuu watapokea zawadi kubwa za Sh. milioni 5, milioni10, na mshindi mkuu Sh. milioni 15,” alisema Bw. Matoi.
Benedict Mwinula, Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali, pamoja na Rodgers Biteko, Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, walishiriki katika droo hii iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Kampeni ya Chanja Kijanja inalenga kuwapa wateja wa Exim fursa ya kushinda kila wanapotumia kadi za Exim kulipia bidhaa au huduma. Hii ni nafasi yako ya kuwa mmojawapo wa mshindi wa Sh. 15 milioni!

  
Dar es Salaam – Katika hafla ya Marketers Night Out iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa, aliwasilisha mada iliyoangazia kwa kina mchango wa programu ya Imbeju katika kubadilisha maisha ya wananchi, hasa wanawake na vijana, kupitia uwezeshaji wa kiuchumi na kukuza ujumuishi wa kifedha nchini.

Akizungumza mbele ya wataalamu wa masoko, viongozi wa taasisi, wajasiriamali na wadau wa maendeleo, Mwambapa alisema Imbeju ni zaidi ya mpango wa kutoa mikopo pekee bali ni programu jumuishi inayolenga kujenga msingi imara wa ujasiriamali. Alieleza kuwa programu hiyo imejengwa juu ya nguzo tatu kuu; elimu ya ujasiriamali na uongozi, upatikanaji wa mitaji rafiki, pamoja na uunganishaji wa wajasiriamali na masoko pamoja na huduma rasmi za kifedha.
 
“Kupitia mafunzo ya vitendo, washiriki huwezeshwa kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi, kutumia fursa za teknolojia, kufuatilia mapato na faida kwa weledi na kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji. mbinu hiyo imewezesha wajasiriamali wengi kuimarisha biashara zao na kuongeza ajira katika jamii”, alisema Mwambapa

Akizungumzia wanawake, Mwambapa alieleza kuwa wamekuwa walengwa muhimu wa programu kwani ndio mhimili wa ustawi wa familia na jamii. Wanawake wengi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za mtaji na elimu ya ujasiriamali sasa wameweza kuanzisha au kupanua biashara zao kupitia Imbeju, jambo lililosababisha kuongezeka kwa uzalishaji, kuboreshwa kwa kipato cha kaya na kuinuka kwa hali ya maisha ya familia zao. Alisisitiza kuwa uwekezaji kwa mwanamke mmoja hupelekea kuleta mafanikio kwa kizazi kizima.

Kwa upande wa vijana, alisema programu hiyo imekuwa chachu ya kubadilisha fikra bunifu kuwa miradi halisi katika maeneo ya teknolojia, kilimo-biashara, sanaa na biashara mtandao. Kupitia ushauri wa kitaalmu, mafunzo na ufadhili wa mawazo bunifu, vijana wengi wamepata uwezo wa kuzifikisha bidhaa zao katika masoko mengi zaidi kupitia majukwaa ya kidijitali, hivyo kuongeza ushindani na kupanua wigo wa biashara zao.
Mwambapa pia aligusia mchango wa Imbeju katika kukuza ujumuishi wa kifedha nchini kwa kuwawezesha wananchi waliokuwa nje ya mfumo rasmi wa benki kufungua akaunti, kujiwekea akiba, kukopa na kufanya miamala kwa urahisi zaidi baada ya kupata elimu ya kifedha. Kupitia ushirikiano wa CRDB Bank Foundation na Benki ya CRDB, huduma hizi sasa zimefika hata maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa huduma za kifedha ulikuwa mdogo awali.

Alisema hatua hiyo imeimarisha uthabiti wa biashara ndogondogo, kuongeza uwezo wa kujitegemea kwa wananchi na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Akihitimisha mada yake, Mwambapa alitoa wito kwa wadau wote kuendelea kuwekeza katika mipango inayowawezesha wanawake na vijana, akisisitiza kuwa mafanikio ya Imbeju ni ushahidi kuwa uwekezaji katika watu ndiyo msingi wa kujenga uchumi jumuishi, thabiti na wenye tija kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhi Tuzo maalumu Meneja Mkazi wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Paul Atallah (wa pili kushoto), kwa niaba ya kampuni hiyo na Qatar Foundation kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kusaidia watu wenye uhitaji.

Na Dotto Mwaibale, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa Tuzo maalum kwa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar na Qatar Foundation kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kusaidia watu wenye uhitaji.

Dkt. Mwinyi alitoa tuzo hizo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu yaliyofanyika Desemba 4, 2025 kwenye Ukumbi wa Dr. Shein – Tunguu, Chuo Kikuu cha SUZA, Mkoa wa Kusini Unguja tukio lililohudhuriwa na viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo, mashirika ya kijamii, na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Zanzibar.

Akihutubia katika maadhimisho hayo Rais Mwinyi aliwataka wadau kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwawezesha watu wenye ulemavu na alisisitiza kuwa maendeleo ya kweli ni yale yanayowahusisha watu wote bila kuacha kundi lolote nyuma.

Aidha, Dkt. Mwinyi alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wadau na wahisani kwa kujitolea kwao kuchangia maendeleo ya jamii zenye watu wenye ulemavu na kueleza kuwa Serikali itayafanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa kamili za kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Paul Atallah, alilishukuru Baraza la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar kwa kutambua mchango wa Emirates Leisure Retail na kueleza kwamba kampuni hiyo itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Serikali na jamii katika kuleta maendeleo chanya kwa watu wenye ulemavu.

Utambuzi wa Wadau Maalumu

Katibu Mtendaji wa Baraza la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, Ussi Khamis Debe, akizungumza kwenye maadhimisho hayo alitoa shukrani kwa wadau wote wanaounga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia watu wenye ulemavu.

Aidha, kwa nafasi ya kipekee alimshukuru Afisa Utawala Msaidizi wa Kampuni ya Emirates Leisure Retail Zanzibar, Ramadhan Hussein Layya (Maarufu Msokolo),kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu, hususan katika kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi kupitia misaada, ushiriki, na michango inayobadilisha maisha ya wanufaika.

Kaulimbiu ya Maadhimisho:

"Uwezeshaji na Ushirikishwaji wa Watu Wenye Ulemavu kwa Maendeleo Jumuishi."

Misaada Iliyotolewa katika maadhimisho hayo kwa ajili ya makundi mbalimbali ya wahitaji ni

Vyerehani kwa ajili ya kujiajiri, kofia maalumu (round hats) kwa ulinzi wa ngozi, miwani ya kinga na vifaa vya kurekebisha uoni, baiskeli za mwendo kwa watu wenye ulemavu wa viungo, fedha za mikopo kwa kuanzisha au kuendeleza biashara.

Vifaa vingine vilivyotolewa ni vya kuongeza uwezo wa kujitegemea mashine za kusaga nafaka.

Misaada hiyo imeleta furaha, matumaini, na thamani kubwa kwa wanufaika na familia zao, ambayo inakwenda kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kuimarisha ustawi wa familia zenye watu wenye uhitaji maalumu.

Kauli ya Emirates Leisure Retail Zanzibar na Qatar Foundation:

Uongozi wa kampuni hizo umeeleza dhamira zao za kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha watu wenye ulemavu Zanzibar wanapata fursa sawa za ustawi na maendeleo, na kuendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii inayobadilisha maisha ya watu wenye uhitaji maalumu.
Viongozi wa Kampuni hizo na wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Dar es Salaam, 30 Novemba 2025: Dhamira ya PUMA Energy Tanzania ya kutoa ubora, ubunifu na huduma yenye kujikita kwa mteja, imethibitishwa kwa matokeo chanya. Usiku wa jana kwenye hafla ya mwaka ya Consumer Choice Awards, baada ya kutunukiwa tuzo mbili kubwa zaidi za usiku huo ambazo ni “Kampuni Inayopendwa Zaidi ya Mafuta na Nishati Barani Afrika” na “Kituo cha Mafuta kinachotoa Huduma kwa Wepesi na Kupatikana kwa urahisi.”

Ushindi huu wa tuzo mbili unaonesha kwamba PUMA Energy si tu kinara katika huduma za rejareja za nishati hapa Tanzania, bali pia katika bara zima la Afrika. Tuzo hizi, zilizopigiwa kura na watumiaji pamoja na wataalamu wa sekta, ni uthibitisho wa mkakati wa kampuni katika kutoa bidhaa bora za mafuta na nishati, mtandao mpana wa vituo vya kisasa, na kiwango cha juu cha utoaji wa huduma.
Tuzo ya “Kampuni Inayopendwa Zaidi ya Mafuta na Nishati Barani Afrika” ni uthibitisho wa taswira chanya ya PUMA Energy barani kote Afrika na picha ya uaminifu, weledi wa kiutendaji, na suluhu bunifu za nishati. Tuzo hii inaonyesha imani ambayo mamilioni ya watumiaji, wafanya biashara, na washirika wanaendelea kuwa nayo kwa PUMA Energy katika shughuli zao za kila siku.

Wakati huo huo, tuzo ya “Kituo cha Mafuta kinachotoa Huduma kwa Wepesi na Kupatikana kwa urahisi.” inaonesha ubora wa utekelezaji wa kampuni hapa nchini. PUMA Energy imewekeza kwa uthabiti kwenye maeneo ya kimkakati, miundombinu ya kisasa, na huduma zinazokidhi mahitaji ya madereva wa kisasa wa Kitanzania kuanzia vituo vyenye mwanga wa kutosha, usalama, usafi wa mazingira, malipo ya kidigitali, hadi mtandao mpana unaohakikisha kituo cha PUMA hakiko mbali na mteja.
Mkurugenzi Mtendaji wa PUMA Energy Tanzania, Fatma Abdallah, alisema:Tunapenda kurudisha shukrani zetu kwa wateja na watumiaji wetu, kwa kutupa sisi nafasi ya kupokea tuzo hizi kubwa. Tuzo hii ya Kampuni inayopendwa zaidi ni mafanikio makubwa yaliyochangiwa na kila mshiriki wa timu ya Puma Enenrgy Tanzania, wauzaji wetu, na wateja wetu wapedwa. Na Tuzo ya Kituo Kinachopatikana kwa Urahisi ni uthibitisho wa kujitoa kwetu na kuhakikisha kila mteja anayeingia kwenye vituo vyetu anapa huduma bila usumbufu, bidhaa za uhakika na kuondoka akifurahi. Tuzo hizi si mwisho wetu, bali zimekuwa chachu ya kutusukuma kuendelea kutoa huduma za viwango vya juu zaidi”

Mwisho, Mkuu wa Sheria na Masuala ya Ushirika wa PUMA Energy Tanzania, Emmanuel G. Bakilana, alisema, “Tunajitahidi kila mara kuhakikisha mteja yupo katikati ya kila tunachofanya.”
Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania PLC, Chiha Nchimbi (wa pili kushoto), akikabidhi kapu la zawadi kwa Rehema Sangaya, mkazi wa Hombolo, Dodoma (wa tatu kushoto), ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za msimu wa Sikukuu. Tukio hilo limefanyika jijini Dodoma jana, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Vodacom kurejesha kwa jamii na kusherehekea wateja katika kipindi hiki cha sikukuu.

Wanaoshuhudia tukio hilo ni pamoja na Meneja Mauzo wa kampuni hiyo wilayani Kondoa Balikulije Mchome, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoyo Julius Magawa (wa pili kulia) na Mtendaji wa Mtaa wa Mkoyo, Pendo Mwijalubi (kushoto).

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni kubwa ya matumizi ya kadi katika msimu wa sikukuu, iitwayo “Chanja Kijanja, Dili Ndio Hili,” ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia 1 Desemba 2025 hadi 31 Januari 2026. Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha Watanzania kupunguza matumizi ya fedha taslimu na kujenga utamaduni wa kufanya malipo ya kidijitali, hususan kwa wateja wanaotumia kadi za Exim Mastercard.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo, alisema kampeni hiyo imeandaliwa ili kutoa suluhisho la malipo lililo rahisi, salama na lenye manufaa kwa wateja katika kipindi ambacho matumizi ya ununuzi huongezeka kutokana na sikukuu.

“Lengo ni kufanya malipo ya kila siku kuwa mepesi zaidi na kuwapa wateja nafasi ya kujishindia zawadi kemkem. Hii inaendana na dhamira ya benki katika kukuza matumizi ya malipo ya kidijitali nchini,” alisema.

Katika kipindi cha kampeni, wateja watakaofanya malipo kwa kutumia kadi za Exim Mastercard kupitia mashine za POS au mtandaoni watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali, ikiwemo:

●Zawadi za kila wiki: TZS 100,000 kwa washindi watano (5).

●Zawadi za kila mwezi: TZS 200,000 kwa washindi kumi (10).

●Cashback maalum katika siku za Black Friday (28 Nov 2025), Cyber Monday (1 Des 2025), na Krismasi (25 Des 2025).

●Zawadi kubwa mwishoni mwa kampeni: TZS milioni 5, TZS milioni 10 na zawadi kuu ya TZS milioni 15.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali wa Exim, Silas Mtoi, alisema kampeni hii ni hatua muhimu katika safari ya taifa kuelekea uchumi unaotumia malipo ya kidijitali.

“Mteja akitumia kadi dukani au mtandaoni anapata usalama, kasi na urahisi. Tunataka kuchochea matumizi ya malipo ya kisasa na kupunguza utegemezi wa fedha taslimu nchini,” alisema Mtoi.

Wateja wa Exim pia watanufaika na zawadi na punguzo maalum katika maduka ya Shoppers na Village Supermarket, pamoja na ofa maalum kwenye migahawa na maeneo ya burudani, ikiwemo Karambezi Café na CIP Lounge katika uwanja wa ndege.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Stanley Kafu, alisema kampeni hii imeundwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wateja katika msimu wa sikukuu.

“Iwe ni maandalizi ya sherehe, safari, kununua mahitaji ya familia au kulipia ada za shule, malipo kwa kutumia kadi ya Exim yanampa mteja urahisi, usalama na nafasi zaidi ya kushinda,” alisema.

Aliongeza kuwa kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa Exim katika kuharakisha mabadiliko ya kidijitali nchini.

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania aliipongeza Benki ya Exim kwa kuendesha kampeni inayoakisi uwazi, ukweli na maslahi ya wateja. Aliahidi kuwa droo zote za washindi zitasimamiwa kwa uadilifu na bila upendeleo.

Kwa mujibu wa Exim, ongezeko la matumizi ya kadi litasaidia kupunguza hatari za kubeba fedha taslimu na kuimarisha mfumo wa kifedha wenye ufanisi zaidi. Benki hiyo imewataka wateja wote kushiriki na kufurahia msimu wa sikukuu kupitia kampeni hii.

Kampeni ya “Chanja Kijanja, Dili Ndio Hili” inatarajiwa kuvutia maelfu ya washiriki huku ikibadilisha namna Watanzania wanavyofanya malipo katika msimu wa sikukuu na hata baada ya msimu huo.

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

Benki ya Exim imejitokeza kuwa mdhamini mkuu wa mbio za Kilomita 5 katika msimu wa nne wa Korosho Marathon, tukio kubwa la michezo lililofanyika mkoani Mtwara likilenga kuhamasisha afya, ustawi wa vijana na mshikamano wa jamii.

Akizungumza wakati wa mbio hizo, mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri wa Vijana, Mheshimiwa Joeli Nanauka, alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wadau mbalimbali katika kukuza afya na maendeleo ya kijamii kupitia michezo. Alisema kuwa michezo ni nyenzo muhimu katika kuibua vipaji, kujenga umoja na kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli chanya za maendeleo.
“Tunazo fursa nyingi kupitia michezo—si tu kuongeza afya zetu, bali pia kujenga mahusiano bora na kuimarisha mshikamano wa kijamii. Tunapongeza Exim kwa kuonesha mfano wa kujitoa katika kuunga mkono juhudi hizi,” alisema Waziri

Kwa upande wake, Exim Bank ilieleza kuwa udhamini huo ni sehemu ya nafasi yake ya kuchangia maendeleo ya jamii na kuunga mkono shughuli zinazowagusa wananchi moja kwa moja. Benki hiyo imerejea dhamira yake ya kuendelea kushiriki miradi yenye manufaa kwa jamii, ikisisitiza kuwa michezo ni jukwaa muhimu katika kuhamasisha maisha bora, kukuza vipaji na kuimarisha umoja wa wananchi.
Kampuni ya Bima ya SanlamAllianz imewashukuru mawakala wao kwa kufanya kazi nao

Akizungumza wakati wa halfa ambayo imefanyika Novemba, 28,2925 jijini Dar-es-Salaam, Meneja mkuu wa biashara na mawakala, Geofray Masige amesema kuwa kampuni hiyo ya SanlamAllianz wanawashukuru mawakala wake kwa mchango mkubwa walioufanya katika kukuza biashara ya bima.

Pia naenda kuchukua nafasi hii kuwatambulisha mawakala watu juu ya muunganiko wetu mpya wa Sanlam na Allianz.
"Mnamo Septemba 2023, kampuni ya Sanlam bingwa wa huduma za bima barani Afrika na Allianz ambao ni miongoni mwa makampuni makubwa zaidi ya bima duniani ziliungana kutengeneza kampuni kubwa ya kifedha isiyo ya kibenki barani Afrika, inayojulikana kama SanlamAllianz.

Hadi sasa, SanlamAllianz ipo katika nchi 26 barani Afrika.

"Muungano huu umeunganisha uzoefu wa pamoja wa zaidi ya miaka 200 barani Afrika na duniani.
Malengo yetu ni kutoa huduma bora zaidi, kuunda bidhaa zinazokidhi matarajio ya wateja, na kujenga jamii inayopata ulinzi wa maisha, fedha, mali, na mafanikio endelevu.

Na hapa ndipo inapotoka kauli mbiu yetu: “Ishi kwa Kujiamini” – Live with Confidence.

Kwa wale old school, sio ile ya kina Msondo na Sikinde hapa tunazungumzia zama za James Bond na Titanic.

"Kufuatia uzinduzi rasmi wa chapa yetu mpya mwishoni mwa mwezi wa kumi, Sanlam General Insurance imeungana na Jubilee General Insurance kuunda SanlamAllianz General Insurance Tanzania.

Vilevile, Sanlam Life Insurance imebadili jina na kuwa SanlamAllianz Life Tanzania.
"Kazi kubwa iliyofanywa na wafanyakazi wenzangu hapa nchini pamoja na wenzetu wa SanlamAllianz Group imetuwezesha kushiriki kikamilifu mabadiliko haya muhimu.

Kwa mujibu wa takwimu za soko la bima nchini.

SanlamAllianz Life inaendelea kuwa kinara katika bima za maisha.

SanlamAllianz General inaelekea kuwa kampuni inayoongoza katika bima za mali kufikia mwisho wa mwaka 2025.

Kwa upande wa General Insurance, tumenufaika sana kupitia muunganiko wa Jubilee Allianz na Sanlam General.

Wafanyakazi wote wanaendelea na majukumu yao kama kawaida, uwezo wetu wa kuandikisha bima (underwriting capacity) umeongezeka, na sasa tunapata utaalamu wa kimataifa kutoka SanlamAllianz Group.

"Hii ni fursa muhimu kwa ukuaji wa soko la bima nchini na pia kwenu ninyi mawakala wetu kwa kuwa ninyi ni sehemu muhimu ya mafanikio haya.

Kwa sasa, SanlamAllianz General Insurance ina takribani mawakala 300 nchi nzima, na lengo letu ni kufikia mawakala 350 ifikapo mwaka 2026.

Mimi na ninyi ni sehemu ya familia hii kubwa ya mawakala wa SanlamAllianz. Mfululizo wa matukio kama haya utafanyika katika matawi yetu yote makubwa ili kila wakala apate nafasi ya kushiriki, amesema,"Masige.

Pia amesema Wana mtandao wa matawi 11, ikiwemo jijini la Mwanza, Arusha, Dodoma, Morogoro, Mbeya, Zanzibar, Moshi, Tanga, Mbagala, Quality Center na Tegeta.
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema kuwa wataendelea kuipa ushirikiano i Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ili kukuza biashara nchini.

Hata hivyo ameipongeza TanTrade kwa utendaji wake katika kuendeleza masoko ya bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi kupitia maonesho ya biashara na misafara ya kibiashara ya kimataifa.

Waziri Kapinga ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi alitembelea ofisi za TanTrade zilizopo jijini Dar es Salaam.

Amesema taasisi hiyo ina mchango mkubwa katika kuwaunganisha wazalishaji wa Tanzania na masoko ya kikanda na kimataifa.

Amesema kuwa jitihada za TanTrade zimeongeza fursa kwa wafanyabiashara, kuchochea kuongezwa kwa thamani ya bidhaa, na kuimarisha utambulisho wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi.

Waziri Kapinga pia aliiagiza mamlaka kuhakikisha wanaboresha mifumo ya kidijitali kuweza kusomana na mifumo mingine ili kurahisisha kwenye upatikanaji wa taarifa za biashara na masoko kwa wadau.

Alisisitiza kuwa upatikanaji wa takwimu sahihi na kwa wakati ni muhimu katika kusaidia maamuzi ya kibiashara na kuongeza ushindani wa nchi katika masoko ya kimataifa.

Aidha, alisema kuwa mfumo mzuri wa utoaji wa taarifa utaharakisha ukuaji wa sekta ya biashara na kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na fursa pana za masoko.

Kwa upende wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Dkt.Latifa Khamis ameaema kuwa ziara ya Waziri wa Viwanda na Biashara wanaenda kufanyia kazi pamoja na kuangali sheria iliyoanzisha Mamlaka hiyo.

Amesema kuwa wamejipanga kufika katika mipaka yote katika kusimamia biashara kubwa ziweze kuendelea kukua na kuleta maendeleo nchini.

Dar es Salaam, 28 Novemba 2025: Benki ya Exim Tanzania na Simba Developers Limited wametia sahihi ya makubalianio ya kimkakati yanayolenga kurahisisha upatikanaji wa makazi kwa Watanzania. Ushirikiano huu unalenga kutoa suluhisho la mikopo ya makazi yenye masharti rahisi kwa wateja wanaponunua nyumba za kisasa zilizojengwa na Simba Developers, kupitia bidhaa ya mkopo ya Exim Bank iitwayo ‘Nyumba Yangu’.

Ushirikiano huu umelenga kujibu ongezeko la mahitaji ya mikopo ya makazi ya bei nafuu katika maeneo ya mijini na pembezoni mwa miji, ambapo wamiliki wengi wa nyumba wanakabiliwa na changamoto za gharama na upatikanaji wa makazi. Kupitia mpango huu, wateja wa Benki ya Exim watafaidika na mikopo ya hadi TZS 1 bilioni chini ya Personal na Preferred Banking, na hadi TZS 1.5 bilioni chini ya Elite Banking, ikiwa na makubaliano nafuu ya riba.

“Kumiliki nyumba ni moja ya mafanikio makubwa kwa Watanzania wengi,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Exim Tanzania Andrew Lymo. “Kupitia ushirikiano wetu na Simba Developers, tunarahisisha safari ya ununuzi wa nyumba kwa kutoa mkopo kwa kadri ya uwezo wako, na kufanya urahisi kwa Watanzania wengi zaidi kufanikisha ndoto zao za kumiliki nyumba.”
Mkurugenzi wa Simba Developers Yusuf Hatimali Ezzi, aliongeza, “Nyumba zetu zimejengwa ili kutoa makazi ya kisasa, salama na ya viwango bora. Kwa kushirikiana na Benki ya Exim tunahakikisha wanunuzi wetu wanaweza kupata fedha kwa haraka na kwa urahisi, na kusaidia familia nyingi ziweze kuishi kwenye nyumba ya ndoto zao.”

Ushirikiano huu unaimarisha nafasi ya Benki katika soko la mikopo ya makazi wakati mahitaji ya huduma za kifedha za makazi kwa ajili ya wateja yanaendelea kuongezeka. Urahisishwaji wa mikopo ya nyumba Benki ya Exim Tanzania na Simba Developers wameongeza viwango vya upatikanaji wa makazi bora na ya kisasa kwa Watanzania.

Aidha, hii inathibitisha dhamira ya Benki hiyo, katika maendeleo ya taifa kwa kupanua upatikanaji wa mikopo ya makazi na kusaidia ukuaji wa makazi bora. 

Kwa wateja wa Benki hiyo, ushirikiano huu unarahisisha upatikanaji wa mikopo ya nyumba, chaguzi sahihi za fedha, na kurahisisha upatikanaji wa nyumba za kisasa kwa mtindo wowote wa maisha na gharama rafiki, Exim Bank na Simba Developers wanawawezesha Watanzania wengi kufanya maamuzi ya kumiliki nyumba kwa kujiamini, kuboresha usalama wao wa kifedha na ustawi wa familia zao.
Puma Energy imemtangaza mshindi wa droo ya vilainishi, ambapo Boaz Aywayo ameibuka na Elite Card yenye thamani ya shilingi milioni 5 ambayo itamuwezesha kufanya manunuzi ya vilainishi au gesi katika kituo chochote cha Puma nchi nzima. Mbali na zawadi hiyo kuu, droo hiyo pia ilizawadia washindi wengine vilainishi na fedha taslimu kama sehemu ya kampeni ya kuwashukuru wateja wa Puma Energy.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa Kitengo cha Oili Puma Energy, Matiko Bugumia, alisema droo hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni kuongeza thamani kwa wateja wake na kuendelea kuhimiza matumizi ya vilainishi halisi. “Soko limekua kwa kasi, lakini changamoto ya bidhaa bandia bado ipo. Ndiyo maana Puma Energy inaendelea kutoa bidhaa bora na salama ili kulinda magari na vifaa vya wateja wetu,” alisema Matiko.
Puma Energy imekuwa ikiwekeza katika kupanua upatikanaji wa huduma zake pamoja na kuelimisha watumiaji kuhusu umuhimu wa kutumia vilainishi halisi vinavyotolewa na vituo rasmi vya mafuta, ili kuepuka athari za bidhaa bandia zinazoongezeka sokoni.

Kwa upande wake, mshindi wa droo, Boaz Aywayo, alishukuru Puma Energy kwa kampeni hiyo na akatoa rai kwa wateja wengine kununua bidhaa kwenye vituo vinavyoaminika. “Bidhaa bandia ni changamoto, lakini Puma Energy imethibitisha kuwa chanzo cha bidhaa salama na zilizothibitishwa,” alisema.

Kampeni ya TUSHAVUKA HUKO ya Benki ya CRDB inaendelea kuvunja rekodi baada ya wateja kutoa ushuhuda kuhusu maboresho makubwa ya mfumo na huduma za benki hiyo, huku wakijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu hadi Shilingi Milioni Moja, Bima ya Afya kwa mwaka mzima, na Bima ya KAVA inayotoa mkono wa pole pale mteja anapopata ulemavu wa kudumu, kufariki au kufiwa na mwenza.

Stephen Adil, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, alisema maboresho yaliyofanywa kwenye mfumo wa Benki ya CRDB yameongeza kasi, usalama na ufanisi wa huduma kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Adili amesema maboresho haya yemeongeza ubora katika huduma zote kuanzia matawini, CRDB Wakala, ATM, pamoja na kwenye majukwaa ya kidijitali ikiwamo SimBanking, Internet Banking, pamoja na majukwaa ya malipo mtandaoni kupitia Lipa Hapa, POS na TemboCard, ambapo sasa huduma zinapatikana kwa usalama wa hali ya juu, na kwa kasi zaidi.”

Kwa upande wa huduma za SimBanking, wateja wengi wamesema huduma zimekuwa na kasi zaidi kuliko mwanzo. Bw. Patrick Msuya, mfanyabiashara wa Kariakoo, anasema SimBanking ndiyo sasa imekuwa “msaidizi wake wa kila siku.”

“Nikituma pesa kwa msambazaji, malipo yanafanyika kwa haraka zaidi. Malipo ya umeme, maji na hata kodi za TRA sasa malipo ni sekunde tu. Nilisikia Benki ya CRDB imeboresha mfumo, lakini sikujua ni maboresho yenye ubora wa kiwango hiki. Tunawapongeza na kuwashukuru sana.”

“Kitu cha kufurahisha zaidi, kila muamala ninaoufanya unanipa nafasi ya kushinda Milioni Moja. Hii imekuwa motisha ya kipekee,” alisema.
Takwimu za benki zinaonesha matumizi ya majukwaa ya kidijitali ya kutolea huduma ikiwamo SimBanking yamepanda kwa kasi tangu kuanza kwa kampeni ya TUSHAVUKA HUKO baada ya kukamilika kwa maboresho ya mfumo, huku malalamiko ya ucheleweshaji au mfumo kukwama yakipungua kwa zaidi ya asilimia 95.

Kwa upande mwengine, huduma za TemboCard nazo zimeendelea kuvutia wateja hasa baada ya Benki ya CRDB kutangaza msimu wa zawadi kwa wanaofanya manunuzi kwenye maduka, migahawa, hoteli, vituo vya mafuta, na sehemu mbalimbali za malipo nchini.

Wikiendi hii, Benki imetua katika maduka ya Shoppers Supermarkets nchini ikiwa na kauli mbiu “Beba TemboCard yako kisha chanja tukuzawadie.”

Bi Stella Nyakato, mkazi wa Mbezi Beach, alikuwa miongoni mwa waliojitokeza kufanya manunuzi. “Nilichanja TemboCard yangu tu baada ya kulipa, Afisa Mauzo wa Benki ya CRDB aliyekuwepo pale akaniambia ‘Hongera, umepata zawadi.’ Sikuamini nilihisi kama benki inanijali binafsi,” alisema kwa shangwe.

“Nimekuwa mteja wa Benki ya CRDB miaka mingi, lakini huu mwaka naona mabadiliko ambayo sijawahi kuyaona. Huduma ni za kasi sana, hata POS hazikati kama zamani.”

Maboresho ya mfumo yaliyofanyika pia yameongeza uwezo wa CRDB Wakala kuhudumia wateja kwa haraka, kupitia utoaji wa fedha, kuweka fedha, malipo ya ankara na huduma nyingine.

“Kasi ya huduma imeongezeka maradufu. Mteja akija, hata kama foleni ipo, ndani ya sekunde chache anahudumiwa. Mfumo haukatiki, na hii imetupa heshima kubwa katika jamii. Wateja wanafurahia zaidi kwa sababu kila muamala pia unawaingiza kwenye droo za zawadi,” anaeleza Bw. Ramadhani Salim, wakala wa CRDB eneo la Kigogo.

Benki ya CRDB imesema promosheni hii itaendelea kwenye maeneo mbalimbali, ikiwawezesha wateja kufurahia ununuzi na kupata zawadi papo hapo.

“Urahisi zaidi, kasi zaidi na ubora zaidi si kauli tu ni uhalisia ambao wateja wetu wanaouona na kuuishi kila siku,” alisema Adili. 

“Kampeni ya TUSHAVUKA HUKO imedhihirisha kuwa huduma bora zinapounganishwa na zawadi, mteja anajisikia kuthaminiwa na kuwa sehemu ya safari ya benki.”

Na Mwandishi Wetu, Babati

Dereva bodaboda wa mjini Babati, Filemon Mbaga, amepewa pikipiki mpya na Kampuni ya Mati Super Brands Ltd baada ya kuibuka mshindi katika challenge ya ubunifu ya kutangaza bidhaa za kampuni hiyo kupitia vyombo vya usafiri.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Chapa wa Mati Super Brands Ltd, Isack Piganio, alisema kampuni hiyo ina utaratibu wa kuthamini watu wanaounga mkono bidhaa zake kwa ubunifu katika maeneo yao ya kazi.
“Tumemchagua Filemon kwa sababu ameonyesha ubunifu wa kipekee katika kubandika nembo na picha za Strong Dry Gin kwenye pikipiki na helmeti yake. Tunatambua mchango wake, na pikipiki hii ni sehemu ya motisha kwa kazi nzuri aliyoifanya,” alisema Piganio.

Aliongeza kuwa challenge hiyo imekuwa ikitumika kama njia ya kuibua vipaji na kuwapa vijana majukwaa ya kujitangaza na kujiongezea kipato, huku akitaja mfano wa Abdul, dereva wa bajaji aliyewahi kuzawadiwa bajaji mpya katika challenge kama hiyo.

Bidhaa za Mati Super Brands Ltd zinazotajwa zaidi sokoni ni pamoja na Strong Dry Gin, Strong Coffee, Sed Pineapple Flavor Gin, Tanzanite Premium Vodka, Tanzanite Royal Gin na Tai Paa Kibabe, ambazo zimeendelea kupata umaarufu kutokana na ubora wake.

Kwa upande wake, Filemon Mbaga aliishukuru kampuni hiyo kwa kutambua juhudi zake na kusema kuwa zawadi hiyo itakuwa chachu ya maendeleo katika maisha yake.

“Nawashukuru sana kwa zawadi hii. Pikipiki hii itanisaidia kuongeza kipato changu, na ninatarajia kujenga nyumba na kusomesha watoto wangu. Nitaendelea kuwa balozi mzuri wa bidhaa za Mati,” alisema Mbaga.

Uongozi wa Mati Super Brands umeendelea kusisitiza kuwa utashirikiana na vijana wabunifu nchini ili kuwapa motisha katika kutangaza bidhaa za kampuni hiyo sambamba na kukuza fursa za maendeleo.
Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto akiangalia bidhaa za Wajasiriamali wa Tanzania katika alipotembelea Maonesho ya 25 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, maarufu kama Nguvu Kazi au Jua Kali, yanayofanyika Nairobi, Kenya tarehe 11 Novemba, 2025 wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo.

Na OWM (KVAU) – Nairobi

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto, amepongeza wajasiriamali wa Tanzania kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora, ubunifu na ushindani mkubwa, alipokuwa akitembelea mabanda ya Watanzania katika Maonesho ya 25 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Nguvu Kazi/Jua Kali) yanayoendelea jijini Nairobi, Kenya.

Akizungumza Novemba 11, 2025, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo, Rais Ruto alisema anavutiwa na namna Watanzania wanavyotumia ubunifu wao kuzalisha bidhaa bora zinazokidhi viwango vya kikanda na kimataifa.

“Wajasiriamali wa Tanzania mmeonesha mfano bora wa ubunifu na ubora wa kazi. Ni wakati sasa wa kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya, Tanzania na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuongeza uzalishaji na kupanua masoko,” alisema Rais Ruto.
Ameongeza kuwa dhamira ya viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha vinavyozuia biashara mipakani, ili kuwezesha ukuaji wa uchumi na ajira kwa vijana.
 
Maonesho yawanufaisha Wajasiriamali

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM), Bi. Alana Nchimbi, alisema maonesho hayo yamekuwa chachu ya maendeleo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati wanaojihusisha na sekta isiyo rasmi.

“Kupitia maonesho haya, wajasiriamali wamepata fursa ya kurasimisha shughuli zao, kutangaza bidhaa, kubadilishana ujuzi na kupata masoko mapya ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Nchimbi.
Wajasiriamali wafurahia pongezi

Wajasiriamali wa Tanzania walionyesha furaha kubwa kufuatia pongezi hizo kutoka kwa Rais Ruto, wakisema zinawapa motisha kuendelea kuboresha bidhaa zao na kupanua biashara zao nje ya mipaka ya Tanzania.

“Tumejifunza mengi kutoka kwa wenzao wa nchi nyingine, tumeona masoko mapya na tumejipanga kutumia fursa hii kuinua bidhaa zetu,” alisema mmoja wa wajasiriamali hao.

Maonesho hayo ya Nguvu Kazi/Jua Kali yamekusanya wajasiriamali kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, yakiwa na lengo la kukuza ushirikiano, ubunifu na maendeleo ya viwanda vidogo barani Afrika.